OPERE NICHOLAS-SIMU YA ELDER

Simu Ya ‘Elder’
Na Opere Nicholas

(Simu inaita. “Elder” anasafisha koo kabla mama hajaichukua)
MAMA:Haloo…unaniskia? Hujambo lakini?
ELDER: Mama hata sikusikii. Nasema jana najuzi na hata ile juzi ingine sijala kitu.
MAMA:Njaa??
ELDER:Njaa mama, jana na juzi na hata ile juzi ingine sijatia kitu kinywani. Credo nipekopa.
MAMA:Njaa iko hata huku. Si ungekopa skuma badala ya “credo?”
ELDER:Nitumie credo.
MAMA:Eee, tumia tu.
ELDER:Nkt! Mama… nipe baba niongee naye.
BABA:Habari yako Opiyo? Ile loan ya HELB imekuja unitumie elfu moja niwalipe watu wakupalilia shamba?
MAMA:(Akizungumza kwa umbali) Mwambie kakaye mdogo hana kiatu.
ELDER: (Akipuuza usemi wa baba) Tafadhali baba, nisambazie hata mia mbili niweze kula leo na kesho.
BABA:Opiyo,maisha ni kuvumilia. Nunua hata mboga ya tano na nyanya ya tano.
ELDER:Hata napirate kwa rafiki, sijamaliza kulipa hela za nyumba.Nisaidieni.
BABA:Kupirate pia iko na pesa, bora usikamatwe. Kwani ile kazi ulikuwa ukifanya Radio Sayari uliipoteza?
ELDER:Ilikuwa attachment. Hainamalipo.
BABA:Mwanangu, malipo ni mbinguni.
ELDER:Wah! Nipe Kaka niongee naye.
KAKA:Hujambo ndugu? Unamalizal ini chuo?Sijamaliza ile sehemu ya nyumba yangu.Niokolee hata mabati tano.
ELDER:Eh! Sasa nitaongea  na nani?
KAKA:Ongea na Shosho.
ELDER:Nkt! Simaanishi hivyo!
SHOSHO:Bwanangu!Jirani yangu Ongoro jana aliacha ng’ombe, mbuzi na kondoowakavamia shamba langu la migomba. Unakuja lini unipeleke kwa chifu?
Kesho?
ELDER:Habari Shosho?
SHOSHO:Ni hayo tu, hayo tu bwanangu. Uniletee blanketi mpya.Ile yangu imekatika vipande viwili.
Asante sana!(Simu inakatika ghafla.Opiyo anabaki kinywa wazi.Hajui aseme nini.)
ELDER: ( Akijizungumzia) Kweli ukiyastaajabia ya mama, baba na hata kaka, utayasikia ya shosho.

The writer is a Kiswahili Editor with The Legacy

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s