Prof. Mazrui Aaga Na OMONDI Joan

Mazrui
Marehemu Ali Mazrui

Wengi waliomjua Profesa Ali Mazrui walimjua kama moja wa waafrika walio na busara na mfahamivu wa ajabu. Marehemu alikuwa ni Profesa wa kiakademia na vile vile mwandishi wa maswala ya kisiasa.Profesa huyu alikuwa mtu mwenye uthabiti na hakuogopa  wala kutishika na jambo lolote lile. Alikuwa mtu mwenye msimamo thabiti na hangeshurutishwa kufanya kile ambacho hakifai kulingana na kaida au kanuni zake.

Mzawa wa pwani, aliyekuwa mjuzi wa maswala ya kidini hasa ya Kiislamu.Aliweza kuandika vitabu vingi vya dini ya kiislamu ambavyo vilichangia sana katika nyanja za kiakademia.

Ni masikitiko kubwa kwa nchi yetu ya Kenya na ulimwengu nzima kwa kumpoteza Profesa Ali Mazrui aliyeipa dunia kisogo mnamo tarehe 12/10/2014 usiku wa jumapili kule Binghamton, New york Merekani alipokuwa akipokea matibabu.Mwendazake Marehemu alikuwa na umri wa miaka 81, alikuwa na wake wawili;Molly Vickerman ambaye pamoja walizaa watoto watano wa kiume. Mke wake wa pili ni Pauline Uti ambaye ni mnaijeria na pamoja walijaliwa kupata wana wawili. Marehemu amewaachia njuma wake wake wawili, watoto watano pamoja na wajukuu. Mwili wake utasafirishwa nchini Kenya kisha atazikwa katika eneo la Ngome ya Yesu, hii ni kulingana na matakwa yake marehemu alipokuwa hai.

Rais Uhuru Kenyatta alituma risala za rambirambi kwa jamaa na marafiki  wa mwendazake.Alisema kuwa anawaombea wote walioathiriwa na kifo hiki ili Mungu aweze kuwaliwaza na kuwafariji katika kipindi hiki. Rais alisema kuwa marehemu Ali Mazrui alikuwa ni mtu wa kupigiwa mfano kwani alikuwa ni mtu mwenye busare na hekima nyingi na kuwa aliheshimiwa kote ulimwenguni. Alisema kuwa pengo lile aliloliacha halitaweza kuzibwa na mtu yeyete yule. Aidha, Seneta wa Mombasa Hassan Omar pamoja na Gavana wa Mombasa Hassan Joho pia waliweza kutumama risala za rambiranbi kwa wote ambao  wameathirika kutokana na kifo hiki cha  profesa Mazrui. Waliweza kumsifia marehemu huyo na wakasema kuwa wamesikitishwa kwa kumpoteza shujaa huyo wa kipwani.

Profesa Mazrui aliweza kusomea katika vyuo vikuu vingi sanaa vya Afrika na hata kimataifa. Baada ya kuhitimu masomo yake alikuwa mwadhiri katikaa chuo kikuu cha Makerere ambapo alikuwa mkuu wa idara ya sayansi za kisiasa. Vile vile aliweza kuwa  Mkuu wa Chuo kikuu cha Jomo Kenyatta. Alikuwa ni mwana Pan Afrika mkuu na alipenda  sana maswala za kisiasa za kiafrika.

Kifo ndicho kudra ya kila mwanadamu bila shaka, kwani hicho ndicho njia ya watu wote. Marehemu amekamilisha wajibu wake duniani. Nasi ambao tungali hai tuweze kuiga mfano wa  marehemu. Tuwe wenye hekuma na ujasiri kama wake. Tuwe wenye msimamo dhabiti na tuweze kuleta mabadiliko katika dunia jinsi mwendazake alivyofanja. Mungu aweke roho yake mahali pema ahera.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s