Heshima Na Taadhima Katika Uchaguzi

Na ALLAN Aguko

Mwanafalsafa wa Kiyunani(Ancient Greek) Plato, amesalia na atasalia siyo tu kwenye kumbukizi za historia , bali pia vinywani mwa wasomi kote ulumwenguni. Alitalii uwanja mzima wa kisiasa na kidemokrasia. Miongoni mwa madai yake sifika ni kuwa ‘’ kwenye uchaguzi tumpigie kura kiongozi bora na wala siye aliye na wafuasi wengi ’. Kitathmini dai hili huzua mdahalo na maswali anuwahi na la kimsingi likiwa ni, Kiongozi bora asiye na wafuasi wengi atashindaje kwenye uchaguzi? Mfanano huu wa Plato utafaa zaidi katika kuhakiki hali kama ilivyo kwenye uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi unaobishia.

Kampeni za kuwarai wanazuo wa Moi zimechacha na kusheheni mnato wa haiba yake. Je, utu wetu utasalia baada ya uchaguzi? Nieleze, mahusiano yetu yatasalia pale pale? Wagombea wengi wamebuni njama na mikakati ya kujihakikishia ushindi. Wengine wanatumia uwezo wao wa mkwanja mrefu ili angalau wapate utambulisho kama sio ushindi. Ni mikakati mizuri pia. Thamani zetu kama wapiga kura na wanafunzi wa chuo kikuu cha Moi katu haziwezi kupigiwa mifano na vileo. Plato alidai ya kwamba viongozi hawa bora wanaweza kutumia njia mibadala ya kuhakikisha wameibuka washindi uchaguzini. Kuwanunulia wafuasi wako vileo huenda ikawa mojwapao wa njia hizi siju lakini. Vileo hutuvua utu na tukasilia watu sawia na mbwa kwa kutoa mihemko na kamsa zisizopendeza masikio. Kwa hivyo mgombea yeyoyte anafaa kutafuta njia nyingine la kujitendea haki kwenye uchaguzi huu.

Tetesi za wagombea wengi kuyatoa mabango ya wenzao na kuyatundika kutani pia zimeshamiri. Wanachokisahau watu wanaofanya tendo hili ovu ni kuwa, wagombea wengine pia ni wapiga kura katika nyadhifa mbalimbali. Mwaniaji wa wadhifa wa ukurugenzi wa burudani na mawasiliano kwa mfano, atampigia kura mwenye kiti, naibu mwenye kiti, katibu mkuu na wengine kwenye msururu huo. Kwa hivyo unafaa kuwaheshimu.

Kumchafulia mpinzani wako jina kwenye mitandao za kijamii kama vile face book pia ni njia ambayo yaelekea kutumika na watu wengi kama alivyopendekeza Plato. Wafuasi wa mwaniaji mmoja, watajaribu kuupunguza umaarufu wake kwa kutunga mambo yasyio. Njia hii mara nyingi badala ya kumchafulia mpinzani wako jina, itamjengea umaarufu hata zaidi kwa kuwa kila mtu atakuwa na raghba za kumfahamu.

Njia moja ya kipekee ninayopendekeza tofauti na ile ya Plato ni, kampeni zenye heshima. Mwanzo kwa mwenyezi Mungu na pili kwa jamii ya wanafuzi. Kuna wanafunzi ambao mara nyingi wameapa kutoshiriki kwenye siasa wala kupiga kura kwenye chaguzi za wanafunzi. Je, utawapa sababu ya kubadili mitazamo yao na kushiriki kwenye uchaguzi? Hili ni swali ambalo kila mgombea anafaa kutilia umuhimu. Mwenendo wako kama mgombea unafaa uwe dhihirisho tosha ya kukupigia kura.

Mazungumzo yako, mahusiano yako, mavazi yako na mienendo yako ndiyo zana kuu itakayokuhakikishia ushindi kwenye uchaguzi. Hakuna yeyote atakayemchagua kiongozi asiyeweza kujieleza na kutoa hotuba mbele ya umati mkubwa wa wanazuo.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s