MAVAZI BY Mannaseh Kuria

Mavazi husitiri miili yetu. Zama za mababu zetu pengiine kabla ya Yesu kuja duniani, mavazi hayakuwa na umuhimu wowote kwa sababu hakukuwa na janaa. Pia maovu yanayotendeka duniani ya uhayawani hayakuwepo. Baadaye yakabuniwa na adinasi akaanza kuyaenzi barabara.
Lakini jinsi ilivyo sasa ni kinyume, mitindo ya mavazi tofauti tofauti imeibuka. Kila kuchao aina yake inazuka. Fasheni za kisasa zinawaathiri hawa vipusa wetu. Ndio kupendeza ni kuzuri na hata macho yetu hupenda kutazama yanayopendeza, mavazi mengine warembo wetu wanayoyavaa hutuacha vinywa vyetu ghaya kushangaa na kupelekea kuvishika vichwa vyetu, fauka ya kukatika shingo tukipenduka. Swali letu ni je, hayo mavazi yanayovaliwa chuoni huvaliwa nyumbani? Bila shaka watajibu la! Hizo nguo hubana nyuma vilivyo, zingine huacha migongo ikiwa wazi bila kusahau mengine huacha ‘ya ng’ombe’ nje. Kwa nini wafanye hayo yote?
Fasheni ni ya muhimu, lazima watu waende na mambo ibuka bila kuachwa nyuma, hapo kitambo shimizi ilivaliwa, leo hii huvaliwa wapi? Fasheni humwacha mtu akiwa safi,nadhifu na hata kupendeza lakini mitindo mingine haifai kwa adinasi aliye na akili timamu kamili.
Wenzi wetu wanapoyavalia hupendeza, mbona nisiwe kama wao?kuwaiga ili tuonekanapo tuwe sawia, lakini wengine hawajui maana ya vazi alilolivaa,kwa mafano ‘ma money grows like grass’ ilhali yeye ni mkata hao ndio utawaona wakivalia nguo za kwenda klabuni kwenda nazo kanisani ambazo zina fedheha.
Tamaa pia hufanya kwenda na mtindo ibuka. Wanaoaadhiriwa haswa ni wasichana, wana tamaa ya kuwavutia wengi, wakizingatia haswa ukoo wa Abrahamu. Ndio, macho hayana pazia. Ukizidisha zaidi utashindwa na hadi kutembea.
Wazazi wetu pengine kwa njia moja au ingine walichangia katika malezi yetu. Wengine walitukazia kuvaa mavazi ya chaguo letu, pengine ni dini au hata kijiji ulicholelewa. Kwa hivyo chuo kikuu kilicho na uhuru, unapelekea kujaribu mavazi yote ili uwe na umahiri.
Swali langu ni je? Visa vya hivi majuzi vya kusikitisha vya kuku Nyeri, wanaume wenye nguvu kupita kiasi bila hata kujali mateke ya punda na hata ng’ombe na p[ia kondoo. Mwingine kashtakiwa huko Thika na nguruwe, mombasani kukawa na mbwa, kesho utamskia paka.ni mavazi ambayo yanavaliwa yanaleta hizi tamaa za kimapenzi hadi inapelekea kukidhia hitaji hilo na mnyama au ni nini? Tunapolijibu swali hili tutafakari pia hulka yetu.
Hapo ndipo utamsikia msichana akisema kuwa anamtaka mwanamme mzuri aliye na tabia nzuri, lakini atampata wapi mwanaume kama huyo wapi ilhali amevalia nguo kama vipande vipande? Twajua vyema kuwa nguo hutuelezea jinsi tulivyo.
Mavazi ya kupendeza ni mazuri lakini tuyavalie kunakotakikana, ya klabu yaende huko ambayo ni mazuri mno, ya kanisa yavalwe kanisani , ya darasani yavaliwe darasani n.k

Mwandishi ni mwalimu mwaka wa tatu

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s