KILICHONIUMA SI HOJA TENA By KURIA Manasseh

Ulikuwa ni wakati wa pata shika katika  kampeni ziliozopita ambapo wanasiasa wa MUSO waliingia kwenye kinyan’ganyiro kilichozua maoni  tofauti. Mikutano ikafanyika ingine isokuwa na ajenda  ilhali ingine ikiwa nayo.  Wagombeaji wakajitosa uwanjani kung’an’gania vitengo mbalimbali,wengine wakatengana na wengine wakashirikiana kuona kwamba wapinzani wao hawawapati ng’o.

Sitauzika kamwe kwenye kaburi la sahau wakati huo kwani mimi na wenzangu tulikuwa wafuasi sugu wa mgombeaji mmoja,walituhimiza tuwakwaruze nao pia watatukwaruze pindi tu watakapoingia kwenye mamlaka. Walitupa ahadi za gangaganga za mganga ambazo humwacha mgonjwa na matumaini. Tuliahidiwa mbingu ambayo hata kipungu hafikii. Baadhi ya ahadi tuliyoahidiwa ni kupata vyumba vya malazi bila matatizo yoyote, usafi utaimairishwa kila mahali haswa ‘mahali mwa usaidizi’,matokeo ya mitihani yatakuwa yakipatikana kwenye mtandao,masomo yataimairishwa ikizingatiwa kuwa baada ya likizo kutia nanga,masomo yalikuwa yakianza baada ya majuma matatu au hata manne, usalama utaimarishwa kwa hali ya juu, pia waliendelea kuongeza chumvi kampeni zao kuwa mambo yanayowazunguka wasomi yatashughulikiwa ipasavyo.

Kilichosemwa kipo na kama hakipo kipo njiani, kilicho baharini kakingoje pwani hatimaye wakajitosa uwanjani  kwa kweli tuliwaweka mizani na kura zikapigwa bila shaka tukawachagua tuliowaona kuwa  wa manufaa zaidi. Baada ya kuvitwaa viti vyao masaibu yalianza. Waliyashughulikia mambo yao wenyewe. Waling’angania maduka na ‘machips café’ ili wajaze mifuko yao iliyokuwa imeraruka raruraru. Vitambi vikaanza kutokeza wakawa nadhifu zaidi. Sisemi ni mbaya kwani maskini akipata matako hulia mbwata. Simu zikawa ukipiga haziingii na zikiingia anadai ako ‘busy al call u laiter’.

Katika masomo mambo yakawa arijojo,kama desturi kuanza kwa  masomo kukawa baada ya majuma matatu au zaidi. Madarasa  hayakushugulikiwa kwani wanachuo wanajaa darasani pomoni hadi kupelekea kuandikia mapajani. Na wale hawana manene iweje?……… usalama tuseme ni rabuka alitulinda kwani mwasi  mkuu mashoka alimaliza masomo yake ingawa hakukosekana visa vya wizi wa laputopu kwenye vyumba vya malazi na maktabani maarufu Afrika mashariki.

Kitengo cha afya kimedorora,usafi katika jumba kuu la ‘H’ na ‘J’ sijui nisemeje?..Vyoo ni vichafu ukiwa na haja barua’inabidi uvumilie nayo. Mwenyekiti akahamia mjini. Chama kikawa kana kwamba hakipo tena, vilio vya wanafunzi vikawa vinagonga kwenye masikio yaliyotiwa nta. Wanafunzi wakileta malalamishi kwa wasimamizi wakuu yanakataliwa kwani mwenyekiti hakuyafuatilia zaidi.

Wanafunzi walihangaika kupata vyumba vya malazi, moi kupata chumba ni kushukuru mola. Mimi nilikiwa nimeahidiwa chumba katika nyumba maarufu ‘A’ ama’B’ lakini ole wangu niliambulia patupu. Wenzangu pia wakavikosa na wakajikuta kuishi “diaspora”. Lakini babu yangu aliniambia hakuna mdogo aliye wa mwisho kabisa.

Hivi sasa mambo yamekuwa tu yale yale ya hapo awali, nimeyazoea kwani siogopi unene wa mbuyu, nilitaka makuu kutoka kwa viongozi hao lakini mambo yalienda arijojo, nimezoea kungoja matokeo ya  mtihani. Mwaka unaisha bila kupata matokeo ya mwaka uliopita, nimejikuna nijipatapo na kuacha mengine yaende vile yatakavyo kwa sababu ukijisumbua na hawa viongozi utashikwa na mpigo wa moyo.

Je tunaowachagua saa hivi watakuwa kama waliopita?  Mambo yatakuwa yale yale ama watabadilisha? Twawaomba wakichaguliwa wawe wakutimiza ahadi zao, na kwa wanachuo wenzangu  masazo ya ndovu majani makavu… tafakari hayo.

 

Mwandishi ni mwalimu mwaka wa tatu

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s