Tunasubiri Vilipuzi Ili Tuanze Kuwajibika ~ Na MUYANZI S Wilson

Tunasubiri Vilipuzi Ili Tuanze Kuwajibika

Huu ndio ujumbe unaopitishwa kimyakimya na wakenya kwa ushirikiano na wadau katika sekta ya usalama hapa nchini. Haya ndio mazoea ya wakenya, kusubiri hadi kutokee janga ndiposa waanze kutapatapa mithili ya mbwa afae maji wakitafuta msaada.  Hivi karibuni taasubi hii imedhihirika hapa chuoni. Hakuna anaejai  kumtambua yeyote aliye karibu naye na makusudio yake ni yapi. Katika  maktaba  yetu,  utepetevu wa usalama umedhihirika kwa kiwango   kikubwa sana. Walinzi wake wamedhihirisha waziwazi ni jinsi gani hawana ujuzi na uzoefu wa kazi za kiusalama. Kama wanao basi wanalaza damu kazini.

Kwa kawaida watu hukaguliwa  waingiapo  sehemu muhimu zinazohitaji ulinzi.  Mikoba yao hukaguliwa ili kuhakikisha kwamba hawana silaha  zozote haramu. Mambo ni kinyume katika chuo cha Moi. Uingiapo maktabani hakuna anayeshughulika  kukutambua na  ni  nini  ulichobeba.  Badala   yake  watakuelekeza mahali pa kuuweka mkoba wako ikiwa unao, lakini utokapo ndani utakutana macho ya walinzi yatakayo kusindikiza na kukupa kwaheri ya kuonana. Huu ndio wakati watapekuapekua mabuku yako au kutoshughulika kamwe. Swali ninalojiuliza ni ikiwa vilipuzi vinaweza kuodolewa maktabani vikipelekwa nje, kando na kuiba vitabu. Ikiwa mfuasi wa kundi haramu la Alshabab ataingia maktabani na vilipuzi  viwili, kimoja katika mkoba na kingine   mfukoni,  atauweka mkoba   wake   mlangoni  wafanyavyo   wanafunnzi na kuingia na kingine hadi vyumba vya juu. Bila    shaka   hatakaguliwa    aingiapo    bali    atakapokuwa akiondoka, au asishugulikiwe na yeyote. Vilipuzi vyake vikilipuka kakutakuwa na mshukiwa maeneo yale. Katika lango kuu la chuo hakuna atakye mtambua kwa sababu mgari hukaguliwa yatokapo, tena kwa kuhesabu wasafiri waliomo. Gari liingiapo hakuna  ukaguzi wa kiusalama unaofanywa na walinzi wetu. Hii inadhihirisha kwamba wanafunzi hapa chuoni ni washukiwa wa kwaza bali sio wageni. Hatua za dharura zichukuliwe kabla ya hatari kutokea.

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s