Waandishi Msilale, asema Bw. Oluoch ~ Na NDONE James

Wanafunzi wa bewa kuu la Moi wamehimizwa wasiache kuandika, kwani jitihada zao hazitaambulia patupu. Akizungumza kwenye warsha ya kuzindua rasmi nembo ya The Legacy iliyoandaliwa katika chumba cha kulia almaarufu Soweto Mess, mfadhili wa toleo la Legacy Bw John Oluoch aliwasihi waandishi wazidi kuandika kwa makini, kwani bidii zao zitalipwa kwa njia moja au nyengine.

“Hapa mnaandika pasi na malipo. Lakini hizi juhudi zenu zitalipwa baadaye,” alisema huku akitoa mfano wa Samuel Siringi ambaye kwa wakati huu anafanya kazi kama mhariri wa gazeti la Daily Nation. Siringi, ambaye alikuwa mwanafuu wa chuo hiki na mhariri wa toleo la Illuminator, ndiye alimpitishia kirungu Bw Oluoch kama mhariri. Naye Bw Oluoch akachukua usukani na kuanza kulihariri toleo hilo.

Alisema kuwa amefurahishwa sana na jinsi uandishi,haswa katika miaka mitano iliyopita, unavyokua hapa bewa kuu.

Akiwapa waandishi zana za uanahabari, aliwaambia watenganishe mbaya, mbovu na mbovu zaidi, kama njia moja ya kuonyesha tofauti ya mwandishi bora na mwandishi ambaye bado yu chunguni.

“Waja hawana wakati wa kusoma mambo ya kawaida. Kama mwandishi mwenye tajriba, unapaswa kuwa na uwezo wa kunusa ni wapi kuna chakula kitamu ambacho ukikipika na ukipakulie watu, watakila na kuagiza cha ziada,” aliongeza.

Aidha alichukua fursa hiyo kuwashukuru waandishi wote wa toleo la The Legacy, haswa kwa ubunifu wao, kuanza kuandika kwa Kiswahili na pia kujumuisha vibonzo au vikaragosi ama ukipenda katuni  katika nakala zao. Alisema kuwa vikaragosi hunena zaidi kuliko picha na huongoa wasomaji sana.

Aliongezea kuwa waajiri waliacha kufuata vyeti wanapotafuta waajiriwa, bali huangalia jambo la ziada na ni lipi uliloweza kufanya lililo tofauti na la mwenzako kutoka chuo kingine.

“Waajiri siku hizi hawaangalii vyeti vya kuhitimu. Wanazingatia vitu tofauti haswa mambo uliyoweza kufanya kama mwandishi. Ulilofanya awali ni ishara ya unaloweza kufanya wakati wa usoni,” aliwaambia waliohudhuria.

Aidha, aliwaonya wanafunzi wasiwe watu wa kuangalia vitu vikifanyika, ama kujitia hamnazo wakati mambo yanatendeka, bali wawe katika mstari wa mbele kuhakikisha kuwa mambo yametendeka.

Ulipofika wakati wa kuzindua nembo ama logo, aliweza kuwaelezea  wanafunzi kuwa ni jambo la busara mtu kujipima mapema na kuanza kuishi kama kielelezo katika jamii. Aliongeza kuwaatakaye  kuwa mwanahabari ni vyema aanze kuishi kama mmoja wa wanahabari.

Baada ya shughuli rasmi kukamilika, ukafika wakati wa maankuli. Baada ya dua fupi kwa Jalali ili akibariki chakula na pia tumbo zitakazokipokea, waliohudhuria walianza kupakuliwa chakula mmoja mmoja. Walipanga foleni na kuhudumiwa na wanadada wa toleo la The Legacy, wakiongozwa na naibu mwenyekiti, Flavia Kassamani. Chapati, nyama na wali. Je, kuna lishe bora kupita hili?

Baada ya matumbo ya waalikwa kuridhika, wanafunzi walijitosa ugani na kuanza kusakata rumba, huku wanadada wakinengua viuno vyao. Hata wale wachezaji wa video ya Bata ya Mzee Yusufu wangeambulia patupu, ingekuwa ni shindano la mchezaji bora.

Naam, kama ulikosa hii hafla hivyo basi ulikosa tamasha la muhula. Vipaza sauti vya Bw Zungu ukumbini, Bw Oluoch ukumbini, wakilishi wa vyumba mbalimbali vya uandishi hapa chuoni, na watayarishaji kipindi waliobobea katika fani hiyo, na baraka za Rabuka zikiwa zimenyunyiziwa kwetu, nani angefanya warsha hii isiwe ya kufana?

Swali langu ni tunaweza kuwa na tamasha kama hili kila Ijumaa?

Kuwa na wiki yenye shughuli nyingi haswa za mijarabu na kujipiga msasa kwani mitihani yazidi kukaribia.

Mwandishi ni Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu, Mawasiliano na Uanahabari.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s