Man U Yarambisha Man City Mchanga – na James NDONE

MATUMAINI ya Man City kuipiku Man U kama wafalme wa mji wa Manchester yalididimia hapo jana baada ya kucharazwa mabao 3-2 na Man U katika uga wa Wembley kwenye kinyan’ganyiro cha Community Shield, kilichohudhuriwa na takriban mashabiki 55,000.
Mechi hii iliwasilisha fursa mwafaka ya kocha wa Man U Bw Alex Ferguson kuonyesha madume alioweza kulamba wakati wa kipindi cha mahamisho, kama vile Ashley Young, Phil Jones na David De Gea, aliyekuwa kipa wa Atletico Madrid ya Uhispania.
Katika kipindi cha kwanza, De Gea alikaribishwa kwenye ligi ya Uingereza kwa bao la kichwa la Joleon Lescot, lililotokana na mkwaju wa adhabu uliopigwa na David Silva. Naam, bao likawa moja bila.Ilipoonekana Man U wametulia, mshambuliaji mahiri wa Bosnia Edin Dzeko alimvurumishia De Gea kombora kali lililopiku urefu wake,dakika moja kabla ya kipindi cha mapumziko. Ilionoekana Man U wanaelekea kupoteza mechi yao ya pili mfululizo katika uwanja wa Wembley dhidi ya Man City. Ni uwanja uu huu ambapo Man City iliicharaza Man U bao moja kwa nunge msimu uliopita katika mchuano wa FA.
Kocha wa Man U alifanya mabadiliko na kuwatoa mabeki wake Rio Ferdinand na kinara wa timu Nemanja Vidic na pia kiungo wa kati Michael Carrick, huku akiwaleta Johny Evans, Phil Jones na Tom Cleverley. Nguvu mpya zilizaa matunda pale Chris Smalling alipomzidia tajriba mlinda lango wa Man City Joe Hart na kufungia Man U bao la kwanza. Ubabe wa Man U ulizidi kudhihirika pale Nani, Cleverley, Young, Welbeck na Rooney walipowakoroga mabeki wa City na Nani akaisawazishia Man U, magoli yakawa 2-2.
Huku penalti zikinusiwa kama mwamuzi mkuu wa magwiji wa mji wa Manchester ni kina nani, winga matata wa Man U, mzaliwa wa Ureno, Luis Nani aliiadhibu City alipodoea kosa la difenda Kompany na kubaki na golkipa. Baada ya fanyafanya na chengachenga zake, alipachika wavuni bao la tatu na la ushindi mnamo dakida ya 94, muda wa ziada, na kuhakikishia Man U ushindi waliokuwa wakiungoja kwa hamu na hamumu. Refa alikipuliza kipenga chake na kuhakikishia Man U ushindi wa 3-2, huku wakitwaa taji lao la kwanza msimu huu.
Mashabiki wa Arsenal, Chelsea na Liverpool walipoona hayo walinyanyua maguu yao na kutoka kwenye ukumbi wa mkutano wa wanafunzi, huku wakibaki na kizungumkuti na hoja zinazokinzana kwani walisikika wakisema, “Manchester United ni wachawi. Wanatumia nguvu za Kiilluminati!”
Changamoto langu ni kwa mashabiki wa Arsenal; nawasihi wajitose kwenye behewa la Man U, kwani ukiwa katika Man U una uhakikisho wa mataji, vikombe na pia kutovunjwa moyo.
Nawatakia juma lisilo na bughudha, doo wala twaa.

Mwandishi ni mwanagenzi wa uwanahabari

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s